• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua hatua kusaidia kampuni kurejesha uzalishaji kwenye maeneo ya biashara huria

    (GMT+08:00) 2020-04-01 10:04:05

    Mashirika ya kuhimiza biashara ya China yamechukua hatua mbalimbali za kuzisaidia kampuni kwenye maeneo ya biashara huria kurejesha uzalishaji mali.

    Kwa mujibu wa Baraza la China la Kuhimiza Biashara ya Kimataifa CCPIT, huduma za kibiashara, kisheria na za kuhimiza biashara zimetolewa na mashirika 11 ya huduma za biashara huria kwa kampuni kwenye maeneo ya biashara huria, ili kuzisaidia kurejesha uzalishaji.

    Mashirika ya mikoa ya Zhejiang, Guangdong na Sichuan na miji ya Tianjin na Shanghai yamezisaidia kampuni zipatazo 200 kupata hati za madhara yasiyoepukika (force majeure certificates), ambazo zinahusisha mikataba yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.81, ili kuzisaidia kampuni hizo kulipa fidia baada ya kushindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa mikataba kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako