• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kurejeshwa kwa uzalishaji mali kwa China kwaanzisha tena ukuaji wa uchumi wa dunia unaodorora

    (GMT+08:00) 2020-04-01 10:34:19

    Takwimu mpya kutoka Shirika la Afya Duniani WHO zimeonesha kuwa, hadi sasa idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona kwenye nchi na sehemu zaidi ya 200 duniani imezidi laki 7, na zaidi ya watu elfu 33 wamefariki. Maambukizi ya ugonjwa huo yameleta athari mbaya kwa uchumi duniani, Shirika la Fedha Duniani IMF limekadiria kuwa ongezeko la uchumi wa dunia la mwaka 2020 litakuwa chini ya asilimia 2.9 ya mwaka 2019. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres pia ameeleza kuwa, uchumi wa dunia utapungua na kuweza kuweka rekodi mpya katika kiwango cha chini zaidi kwenye historia. Kutokana na hali hii, China ikishikilia wazo la Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, inashughulikia kazi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini, huku ikihimiza kurejeshwa kwa uzalishaji mali, na kuchangia ukuaji wa uchumi wa dunia unaokaribia kusimama hatua kwa hatua.

    Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya Soko la Kimataifa kwenye Wizara ya Biashara ya China Bw. Bai Ming ameeleza kuwa, China ni nchi kubwa kiuzalishaji, kurejeshwa kwa uzalishaji mali kwake kunachochea maendeleo ya uchumi. Kwa uchumi wa dunia, China inachukua sehemu muhimu kwenye mnyonyoro wa viwanda na utoaji wa bidhaa duniani, kurejeshwa kwa uzalishaji mali kwa China kumetoa nafasi za ajira na kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa nchi zilizoko kwenye minyororo hiyo duniani.

    Tarehe 27 Machi, mkutano wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China pia ulisisitiza ulazima kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi na kibiashara, kuharakisha ujenzi wa mfumo wa mnyororo wa ugavi wa kimataifa, na kuhakikisha uchukuzi wa kimataifa wa bidhaa unafanyika kwa utaratibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako