• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha kuchunguza sayari ya mwezi cha China chatembea zaidi ya mita 424 kando ya sayari ya Mwezi

    (GMT+08:00) 2020-04-01 17:53:42

    Chombo cha kuchunguza sayari ya Mwezi cha China, Yutu-2 kimetembea mita 424.455 upande wa mbali wa sayari hiyo ili kufanya utafiti wa kisayansi wa eneo hilo jipya.

    Kituo cha Mradi wa Utafiti wa Mwezi na Anga ya Juu kilicho chini ya Idara ya Anga za Juu ya China kimesema, vyombo vyote vinavyoongozwa na Chang'e-4, vimemaliza kazi yao katika siku ya 16 katika mwezi, na kujizima kwa ajili ya usiku kutokana na ukosefu wa nguvu ya umeme wa jua.

    Yutu-2 kimefanya kazi kwa muda mrefu zaidi ya miezi mitatu iliyopangwa, na kuwa chombo cha kwanza kilichotembea kwa muda mrefu zaidi kwenye sayari ya Mwezi. Chombo hicho kimewasaidia wanasayansi kugundua siri zilizofichwa chini zaidi pembezoni mwa sayari hiyo, na kutoa uelewa mpya kuhusu mabadiliko ya kijiolojia ya Mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako