• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya kesi za COVID-19 duniani yazidi laki 7.5

    (GMT+08:00) 2020-04-01 18:04:13

    Takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO zinaonyesha kuwa, mpaka saa sita usiku wa tarehe 31, mwezi uliopita, idadi ya jumla ya maambukizi ya virusi vya Corona dunian ilifikia 754,948 na watu 36,571 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

    Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha The Johns Hopkins zinaonyehsa kuwa, mpaka saa tano usiku, jana, Marekani ilikuwa na kesi 181,099 za virusi hivyo, na watu 3,606 wamefariki.

    Nchini Italia, idadi ya kesi za virusi hivyo imefikia 105,792 na kusababisha vifo 12,428.

    Wizara ya afya ya Ufaransa jana imetangaza kuwa, nchi hiyo ina kesi 52,128 za virusi vya corona, na watu waliofariki kutokana na virusi hivyo ni 3,523.

    Takwimu iliyotolwa na wizara ya afya na huduma za jamii ya Uingereza imesema, Uingereza ina kesi 25,150 za virusi vya corona, na watu 1,789 wamefariki kutokana na maambukizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako