• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya: Uzalishaji wa mafuta wa kila siku nchini Libya wapungua

    (GMT+08:00) 2020-04-01 18:55:03
    Uzalishaji wa mafuta wa kila siku nchini Libya umepungua kutoka zaidi ya mapipa milioni 1.2 hadi mapipa chini ya 80,000 kutokana na kufungwa kwa bandari za mafuta.

    Shirika la Mafuta la Kitaifa limesema ufungaji huo unafanywa na viongozi wa kabila la mashariki kupinga dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

    Limesema kuwa ufungaji huo umesababisha hasara ya dola bilioni 3.8 tangu Januari 17.

    Kampuni ya kitaifa ya mafuta imesema inawataka wale waliohusika na kufungwa kwa haramu kukomesha kitendo hicho ili kuinusuru sekta ya mafuta, wafanyikazi wa sekta hiyo pamoja na raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako