Katika taarifa ya Katibu Mkuu wa shirika hilo Mukhisa Kituyi alisema wakati ulimwengu unapambana na janga hilo, tasnia ya uchukuzi wa baharini duniani inachukua jukumu muhimu kutoa mchango wake.
Kituyi amesema karibu asilimia 80 ya biashara ya kimataifa hutegemea uchukuzi wa baharini kusafirisha chakula, nishati na malighafi za ulimwengu.
Alisema kuwa katika wakati huu wa mzozo duniani, ni muhimu zaidi kuweka minyororo ya usambazaji wazi na kuruhusu biashara ya baharini na usafirishaji baiana ya nchi kuendelea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |