• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CORONA: Ronaldo aitwa "mzururaji" na kuamriwa aondoke mjini Madeira

  (GMT+08:00) 2020-04-02 08:42:44

  Cristiano Ronaldo ameitwa "mzururaji" na kuamriwa aondoke katika mji wa Madeira nchini Ureno na mwanasiasa mmoja baada ya picha kuibuka zikimuonyesha nyota huyo wa Juventus akitembea mitaani na familia yake wakati huu wa janga la ugonjwa wa corona. Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun ya Uingereza, mwanasiasa huyo, Rafael Macedo, alimshambulia vikali Ronaldo katika mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya kuona picha zake akiwa anatembea na mpenzi wake Georgina Rodriguez na watoto wao katika mji huo ambao ndipo mwanasoka huyo alipozaliwa. Alkiandika na hapa nanukuu "Namtaka mnyama huyo aliyekuja kutoka Italia kukaa nyumbani. Niondoleeni mzururaji huyo katika mji wa Madeira." Lakini katika andiko lingine katika Facebook, Macedo alisema akaunti yake ilidukuliwa hawezi kutoa kauli mbaya kama hiyo dhidi ya CR7 wao. Hii sio mara ya kwanza jambo kama hili kutokea, na ameshabadilisha password zake. Aidha katika hatua nyingine alichukua fursa ya kumuomba radhi kila mtu hasa Ronaldo na familia yake ambao amesema anawathamini sana, kwa kile kilichotokea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako