• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maambukizi ya COVID-19 kote duniani kufikia milioni 1 ndani ya siku kadhaa

    (GMT+08:00) 2020-04-02 09:02:40

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Bw. Tedros Ghebreyesus amesema kuenea kwa kasi kwa virusi vya Corona kumesababisha ongezeko kubwa la maambukizi katika wiki kadhaa iliyopita, na idadi hiyo itafikia milioni 1 ndani ya siku kadhaa na idadi ya vifo itazidi elfu 50.

    Bw. Tedros ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la kasi na kuenea kwa virusi hiyo duniani. Amesema wiki iliyopta, idadi ya maambukizi imeongezeka zaidi ya mara moja, na kuenea katika nchi na sehemu zote duniani. Amesema katika siku kadhaa zijazo, idadi ya maambukizi itafikia milioni 1 na idadi ya vifo itazidi elfu 50.

    Ameongeza kuwa ingawa idadi ya maambukizi barani Afrika, Amerika ya Kati na Amerika ya kusini ni ndogo, WHO inaona maambukizi ya virusi vya Corona huenda yataleta athari mbaya kwa jamii, uchumi na siasa katika sehemu hizo. Bw. Tedros ametoa mwito wa kuzisaidia nchi hizo kuinua uwezo wa kugundua, kupima, kuweka karantini na kutibu wagonjwa, na kufuatilia watu walio karibu na wagonjwa hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako