• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN: Ukuaji wa uchumi wa dunia kupungua kwa asilimia moja mwaka huu kutokana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-02 10:15:21

    Ripoti iliyotolewa jana na Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA imeonyesha kuwa, ukuaji wa uchumi wa dunia unaweza kupungua kwa asilimia moja mwaka huu kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona unaokithiri kote duniani, hali ambayo itakuwa mbaya zaidi kama hatua za kifedha zenye ufanisi hazitachukuliwa.

    Ripoti hiyo imesema takriban nchi 100 zimefunga mipaka, mamilioni ya wafanyakazi wangepoteza kazi zao, hali ambayo inamaanisha ukuaji wa uchumi wa dunia utapungua kwa asilimia 0.9 hadi mwishoni mwa mwaka huu, na idadi hiyo inaweza kuwa kubwa kama serikali za nchi mbalimbali hazitachukua hatua za kuchochea ukuaji wa uchumi.

    Makadirio yanaonyesha kuwa sekta ya huduma katika nchi za Ulaya na Amerika ya Kaskazini inaathiriwa zaidi na virusi vya Corona, sekta ambayo inatoa zaidi ya robo ya nafasi zote za ajira katika nchi hizo. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukua hatua madhubuti za kifedha za kuchochea ukuaji wa uchumi, ambazo zinatoa kipaumbele katika matumizi kwenye huduma za afya na kuziunga mkono familia zinazoathiriwa zaidi na mlipuko wa COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako