• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la WHO lapinga baadhi ya vyombo vya habari kulaumu kuwa takwimu zilizotolewa na China si wazi

    (GMT+08:00) 2020-04-02 11:45:08

    Shirika la Afya Duniani WHO huko Geneva limefanya mkutano na wanahabari kuhusu virusi vya Corona na kupinga baadhi ya vyombo vya habari kulaumu takwimu zilizotolewa na China kuwa si wazi.

    Mkuu wa mradi wa dharura wa shirika hilo Dkt Mike Ryan amesema, takwimu zinazotolewa kila siku na nchi mbalimbali zina ushahidi mwingi wenye msingi wa kisayansi. Shirika la WHO litashirikiana na kila nchi, ili kupata takwimu nzuri zaidi. Wakati huohuo, tunapaswa kufahamu kwamba chini ya hali ya shinikizo, ni vigumu kwetu kupeana habari na takwimu zinazobadilika kila dakika.

    Ameongeza kuwa hivi sasa, shirika hilo limepata habari za utafiti kuhusu kuenea kwa virusi kutoka nchi mbalimbali, ambazo ni pamoja na moja kutoka Singapore, moja kutoka Ujerumani, moja kutoka Marekani na nne kutoka China. Ameshukuru nchi hizo zote kwa kutoa takwimu hizo katika kipindi cha mwanzo cha maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako