• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eritrea yaweka zuio la siku 21 kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-02 20:40:36

    Wizara ya Habari nchini Eritrea imetangaza marufuku ya kutotoka nje kwa muda wa siku 21 ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, wananchi wote wanapaswa kukaa majumbani kwao kwa siku 21 kuanzia leo, lakini marufuku hiyo haitahusisha watu wenye majukumu ya muhimu ya kimaendeleo.

    Pia wizara hiyo imesema, wanafamilia, wasiozidi wawili kwa wakati mmoja, wanaruhusiwa kwenda kufanya manunuzi ya vyakula wakati wa mchana.

    Mpaka sasa idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona nchini humo ni 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako