• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu Tanzania aeleza mafanikio yaliyopataikana ndani ya kipindi cha miaka mitano

    (GMT+08:00) 2020-04-02 20:40:55
    Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano mafanikio makubwa yamepatikana na yamesaidia kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii katika taifa hilo.

    Alieleza mafanikio hayo jana wakati akiwasilisha hotuba yake kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka 2020/2021.

    Aliyataja mafanikio hayo kuwa ni ujenzi wa miundombinu muhimu ya kiuchumi hususan ya usafiri na usafirishaji sambamba na uimarishaji wa huduma muhimu za kijamii ni miongoni mwa masuala yaliyopewa kipaumbele.

    Aliyataja kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa, ufufuaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), ufufuaji wa mali za ushirika mfano, UCU SHIRECU na Mamlaka ya Mkonge Tanzania na ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere.

    Alisema pia ulinzi wa maliasili na rasilimali na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu, afya na maji ni kati ya hatua za msingi zinazochukuliwa na serikali ya Rais Magufuli katika kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako