• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia atoa msamaha kwa wafungwa 148 ikiwa ni juhudi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-02 20:41:00

    Rais Mohamed Farmajo wa Somalia, leo ametoa msamaha kwa wafungwa 148 ikiwa ni sehemu ya hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona nchini humo.

    Rais huyo amesema, kuachiwa kwa wafungwa hao waliofanya makosa madogo kunafuatia ripoti iliyowasilishwa kwake na mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu hali ya wafungwa nchini humo wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona.

    Pia rais Farmajo amezielekeza mamlaka za magereza na wizara ya afya kuchukua hatua mwafaka kuzuia mgogoro wa kiafya kwa wafungwa waliobaki gerezani.

    Mpaka sasa, kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Somalia zimefikia tano, zikiwa ni raia watatu wa Somalia na raia wawili wa kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako