• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini na China zajadili juhudi za pamoja za kukabiliana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-03 10:02:41

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini jana alikutana na balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Hua Ning, na kuipongeza serikali ya China kwa kuchukua hatua zenye ufanisi katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, na kujatahidi kuziunga mkono nchi zote duniani kwenye vita hiyo.

    Balozi Hua Ning amesema ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umeichangia fedha kwa ofisi ya Shirika la Afya Duniani WHO nchini humo kwa ajili ya kununua vifaa vya matibabu, msaada kutoka kwa makampuni mbalimbali ya China umepelekwa Juba. China itaendelea na mawasiliano ya karibu na wizara ya afya ya Sudan Kusini na ofisi ya WHO nchini humo, ili kuisaidia nchi hiyo katika kuongeza uwezo wa kupambana na virusi.

    Hadi sasa Sudan Kusini hajaripoti mgonjwa wa COVID-19. Kwa mujibu wa kamati ya serikali ya nchi hiyo ya kukabiliana na ugonjwa huo, Sudan Kusini imekuwa na uwezo wa kupima virusi vya corona, tayari imejenga kituo cha karantini na kutibu wagonjwa, imeunda timu ya kukabiliana na maambukizi na madaktari na wauguzi waliopata mafunzo husika wako tayari. Katika eneo la mpakani, vimewekwa vituo vya ukaguzi na mfumo wa kufuatilia pia umeanza kufanya kazi katika maeneo ya makazi na hospitali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako