• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU na China zajadili kuimarisha uratibu kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-03 10:04:32

    Naibu mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Kwesi Quartey ameipongeza China kwa kufanikiwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona na kuisaidia Afrika katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo.

    Bw. Kwesi alisema hayo alipokutana na balozi wa China katika Umoja wa Afrika Bw. Liu Yuxi katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

    Mazungumzo hayo yalihusu namna ya kuimarisha uratibu kati ya Umoja wa Afrika na China, katika kukabiliana na virusi vya corona barani Afrika. Pia walijadili kufanya ushirikiano zaidi katika fani ya afya ya umma na kupunguza athari za ugonjwa huo kwa jamii na uchumi katika nchi za Afrika na watu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako