• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara kati ya China na nchi za nje yaanza kufufuka

  (GMT+08:00) 2020-04-03 10:45:46

  Wakati biashara ya kimataifa inaathiriwa vibaya na maambukizi ya virusi vya corona, uchukuzi wa mizigo wa reli kati ya Wuhan na miji ya Ulaya umerejeshwa katika hali ya kawaida, huku matunda kutoka nchi za Kusini Mashariki mwa Asia yanasafirishwa kuja kwenye soko la China kwa njia ya reli. Takwimu kutoka forodha ya Hangzhou, mji wa pwani mashariki mwa China, zinaonyesha kuwa maombi ya kusafirisha nje bidhaa yanaongezeka kwa kasi, na bidhaa nyingi zinaelekea kwenye soko la Ulaya, ikiwemo Russia, Hispania na Ufaransa.

  Kwa mujibu wa uchambuzi wa picha zilizopigwa na satelaiti uliofanywa na kampuni ya Orbital Insight ya Marekani, toka katikati ya mwezi Machi, katika bandari ya Shanghai, ambayo ni bandari kubwa zaidi ya biashara duniani, idadi ya meli zinazoondoka kutoka bandari hiyo inaongezeka kwa kiasi kikubwa. Kutokana na hali hii, pilikapilika zinaanza kurejea katika bandari mbalimbali duniani. Bandari ya Singapore ambayo ni bandari kubwa ya pili duniani na bandari ya Rotterdam ya Uholanzi, zinarejesha kazi. Kampuni kubwa zaidi ya makontena duniani Maersk imesema, "kwa sababu China iko tayari kupokea meli, uchukuzi wa mizigo katika bandari mbalimbali ikiwemo Rotterdam unaanza kufufuka.".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako