• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juhudi za kukabiliana na COVID-19 zahitaji sauti chanya zaidi

    (GMT+08:00) 2020-04-03 20:46:12

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, juhudi za kukabiliana na COVID-19 zinahitaji sauti tulivu, chanya na zenye busara.

    Hua Chunyin amesema hayo kufuatia barua ya wazi iliyochapishwa katika jarida maarufu la The Diplomat iliyoandikwa na wasomi 100 wa China kwa jamii ya Marekani, ambayo imetoa wito wa mshikamano na ushirikiano duniani kufuatia mawazo ya jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja, ili kukabiliana na virusi vya Corona.

    Hua amesema, kama nchi nyingine, China pia imeathiriwa na virusi hivyo, na watu wa nchi mbalimbali duniani wanapaswa kushikamana na kushirikiana, ili kushinda virusi hivyo mapema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako