• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kipindi maalum cha kujadili changamoto ya virusi vya Corona katika Siku ya Qingming

    (GMT+08:00) 2020-04-04 07:43:07

    Tarehe 4, Aprili kwa mwaka huu ni Siku ya Qingming hapa China. Hii ni siku maalum ambayo inatengwa na China kila mwaka kuwakumbuka marehemu. Katika siku hii wachina wote wanapewa mapumziko ya siku moja ili kufanya shughuli za kuwakumbuka marehemu wao wapendwa, mashujaa na watu wengine.

    Leo Jumamosi ni siku ya maombolezo ya kitaifa ambapo baraza la serikalai la China limeitanganza siku hii kuwa ni siku ya kuwakumbuka watu waliokufa kutokana na ugonjwa huu. Leo bendera za kitaifa zinapepea nusu mlingoti katika nchi nzima na kwenye balozi zote za China nje ya nchi, na shughuli za burudani za umma zitasimamishwa kote nchini. Saa nne asubuhi umetajwa kuwa ni muda kwa wachina wote kukaa kimya kwa dakika tatu kuwakumbuka waliokufa, na ving'ora na honi za magari, treni na meli vitasikika kuomboleza.

    Mwaka huu siku hii sio ya kawaida, kwani idadi ya watu wanaokumbwa imeongezeka kwa ghafla kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona. Kuna wachina wengi ambao inawezekana kuwa hii ni mara yao ya kwanza kutembelea makaburi kutoa heshima kwa jamaa zao waliofariki kutokana na virusi vya corona. / Lakini janga hili si kama tu limeikumba China. Tunasikia tafrani katika bara zima la Ulaya, Amerika Kaskazini na kusini, na hapa Asia, na hata kwenye nchi za Afrika ambapo hadi sasa ni sasa ni nchi tano tu Comoros, Lesotho, Sao Tome ana Principe, Malawi na Sudan Kusini ndio zinaaminika bado havijafikiwa na virusi. / Takwimu kutoka Shirika la Afya duniani WHO zinasema tayari watu milioni 1 wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona kote duniani, na wengine elfu 50 kati yao wamefariki dunia.

    Bara la Afrika bado halijaathiriwa sana na virusi vya Corona, lakini mwelekeo uliopo sasa ni kuwa kama hatua makini hazitachuliwa, basi tunayosikia Ulaya na Marekani tunaweza kuanza kuyasikia kwenye nchi za Afrika.

    Kila linapotokea janga duniani kuna hali kadhaa zinajitokeza, kwanza huwa tunaona watu wenye ubinadamu na wasio na ubinadamu, tunaona wenye busara na wasio na busara, na tuona wenye elimu na wasio na elimu. Kilichopo ni kuwa changamoto ya virusi vya Korona ni kuwa inatutaka sote bila kujali rangi zetu, nchi zetu, vyeo vyetu, umri na hata jinsia tuwe katika mstari mmoja, ndipo tunaweza kushinda vita hii.

    Lakini hali halisi inaonyesha tofauti, licha ya wataalam kutoa maelekezo baadhi wanapuuza, badala ya kueneza habari za kweli na zenye ushahidi wa kisayansi, watu wamekuwa wakitumia ovyo mitandao ya kijamii kueneza habari zisizo na msingi na kutatanisha mapambano dhidi ya virusi vya Korona. Kujadili haya ni pamoja na Fadhili Mpunji, Han Mei, Pili Mwinyi na Hassan Zhou. Pia kuna George Njogopa mwandishi wetu kutoka Dar es salaam, John Kibego mwandishi wetu kutoka Uganda, na Mwanahabari Eric Bigeon kutoka Kenya ambao wataungana nasi kwa njia ya simu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako