• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa IMF yatahadharisha kuhusu uchumi kudorora zaidi kuliko msukosuko wa fedha duniani mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2020-04-04 18:50:48

    Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Kristalina Georgieva ametahadharisha kuhusu kudorora zaidi kwa uchumi kuliko ilivyokuwa wakati wa msukosuko wa kifedha duniani uliotokea mwaka 2019.

    Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa pamoja na Shirika la Afya Duniani WHO jana mjini Geneva, Bibi Geogieva amesema misukosuko miwili ya kiafya na kiuchumi inayosababishwa na virusi vya Corona haijawahi kutokea katika historia ya IMF. Amesisitiza kuwa kuokoa maisha ya watu na kulinda shughuli za watu kujikimu kimaisha vinapaswa kufanywa kwa pamoja wakati virusi hivyo vinasambaa kote duniani.

    Bibi Geogieva ameeleza kuwa IMF inatumia ipasavyo uwezo wake wa kifedha wa dola za kimarekani trilioni moja na karibu dola bilioni 90 zimepelekwa kwenye masoko yaliyojitokeza hivi karibuni na nchi zinazoendelea zilizoathiriwa zaidi na janga hili la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako