• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump aunga mkono kufukuzwa kazi kwa nahodha wa manowari ya kuchukulia ndege iliyokumbwa na Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-05 18:54:27

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaunga mkono kuondolewa kwa nahodha Brett Crozier wa manowari ya kuchukulia ndege ya Uss Theodire Roosevelt, ambayo imekumbwa na mlipuko wa COVID-19.

    Akiongea na wanahabari Ikulu Trump amesema barua ya Crozier ya kuomba msaada kutoka kwa wakuu wake ili kudhibiti virusi vilivyoenea kwenye chombo hicho ilikuwa mbaya. Amesisitiza kuwa haoni kuwa ni sahihi kuandika barua yenye kurasa tano kutoka kwa nahodha na kuisambaza kila mahali.

    Katika barua hiyo aliyoituma kwenye kundi la meli la Navy Pacific mapema wiki hii, nahodha huyo ameomba wizara ya ulinzi kuharakisha kuondoa asilimia 90 ya wafanyakazi na kuwapeleka kwenye karantini kwa wiki mbili huko Guam, la sivyo watashindwa kushughulikia vizuri mali walizokabidhiwa.

    Ikiwa imetia nanga huko Guam, hadi kufikia Jumamosi Roosevelt ina wagonjwa 155 wa virusi vya Corona, wakiongezeka kwa asilimia 13 katika saa 24, na asilimia 44 ya wafanyakazi 5000 waliomo kwenye manowari wamepimwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako