• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ambundo: Corona imechelewesha ubingwa wa Gor Mahia

  (GMT+08:00) 2020-04-06 16:59:24

  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Dickson Ambundo anayeichezea kwa mkopo Gor Mahia ya Kenya akitokea timu ya Alliance FC ya Mwanza, amesema kama sio janga la Corona huu ulikuwa ni mwezi wa kujihakikishia kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Kenya, KPL. Ambundo amesema, itabidi wasuniti hadi hali ikiwa shwari ili kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Kenya kwa mara nyingine tena, na utakuwa ubingwa wake wa kwanza akiwa na miamba hiyo ya soka nchini Kenya. Gor Mahia maarufu K'Ogalo wanaongoza msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 54 ambazo wamezipaka katika michezo 23, huku Kakamega Boys waliwafuata wakiwa na point 47. Wakati huohuo, rais wa Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF) amesema Gor Mahia inapaswa kutangazwa kuwa bingwa wa Ligi Kuu nchini humo kwa msimu huu kama mashindano hayo hayatarejeshwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako