• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Lingard akomaa Manchester United akataa kwenda Arsenal

  (GMT+08:00) 2020-04-07 16:17:47

  Kiungo wa timu ya Manchester United, Jesse Lingard amesema atabaki katika timu hiyo apiganie nafasi na hata kama atakaa benchi sio mbaya, lakini hayuko tayari kujiunga na Arsenal. Lingard amesema, hana mpango na wala hajawahi kushawishika kujiunga na Arsenal, ambao wamedaiwa kuhitaji saini ya kiungo huyo wakati dirisha la usajili la msimu wa kiangazi litakapofunguliwa. Huu ni mwaka wa mwisho wa mkataba wa Lingard katika timu ya Manchester United na tayari ameonekana kufutwa kwenye mpango wa kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer. Inadaiwa kuwa, kocha huyo ana mpango wa kuondoa wachezaji wa ziada kwenye kikosi chake ili kupata pesa za usajili, huku Pauni milioni 30 zinaripotiwa kuwa zitatosha kumng'oa Lingard kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako