• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya kaunti ya Machakos kuondoa bili zote za maji kwa matumizi ya nyumbani kuanzia Mei 1 hadi Desemba 31.

    (GMT+08:00) 2020-04-07 17:32:12

    Gavana wa Machakos Alfred Mutua amezitaka kampuni zinazotoa umeme na maji kuondoa bili za matumizi ya nyumba kwa miezi sita.

    Mutua amesema hii itasaidia Wakenya nyakati hizi ngumu za uchumi kutokana na janga la coronavirus ambalo limepata nchi nyingi ulimwenguni.

    Gavana amependekeza umeme unaweza kuwa hadi kiwango fulani cha matumizi ambayo inatosha kwa matumizi ya nyumbani kama vile matumizi ya taa na matumizi mengine ya nyumbani.

    Gavana huyo aliongezea kwamba kusimamishwa kwa bili za umeme haitaathiri vibaya kampuni ya umeme ya Kenya Power kifedha, akiongeza kwamba msambazaji wa umeme anaweza kumudu malipo kwa muda mrefu zaidi.

    Mutua amesema serikali yake ya kaunti ya Machakos itaondoa bili zote za maji kwa matumizi ya nyumbani kuanzia Mei 1 hadi Desemba 31.

    Alisisitiza Hazina ya Kitaifa kuondoa malipo ya VAT kwenye gesi ya kupikia na mafuta ya taa ili kuruhusu wakenya kutumia pesa walibakia nayo kwa bidhaa zingine muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako