• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: FIFA yatolea ufafanuzi sintofahamu ya vilabu na mikataba ya inayomalizika ya wachezaji wao

  (GMT+08:00) 2020-04-08 09:24:13

  Baada ya kuwa katika hali ya sintofahamu kwa vilabu mbalimbali vya soka kutokana na kusimama kwa Ligi huku baadhi ya wachezaji wao wakiwa wanamaliza mikataba, Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA limelitolea ufafanuzi sula hilo. Awali vilabu vilikuwa vinawaza kwamba kabla ya kusimama kwa ligi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, ilikuwa imalizike Mei na wachezaji wengine walikuwa wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa mwezi Mei hivyo msimu wangemaliziaje. FIFA imeeleza kuwa kutokana na changamoto iliyojitokeza ni wazi sasa wataruhusu kwamba ili mkataba wa mchezaji na klabu uhesabike umemalizika kwa msimu huu, ni pale tu msimu wa mashindano 2019/2020 utakapokuwa umemalizika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako