• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: KWS yaondoa pendekezo la kuongeza ada

    (GMT+08:00) 2020-04-08 18:50:51

    Shrika la kuhudumia wanyamapori nchini Kenya KWS limeondoa tangazo la awali la kuongeza ada za kuingia kwenye hifadhi za wanyama nchini humo.

    KWS ilikuwa imetangaza kuwa itaongeza ada hizo kwa wakenya kwa asilimia 300 kuanzia mwezi Julai.

    Hata hivyo sasa ada iytasalia kama awali baada ya malalamishi kutoka kwa watalii wa ndani.

    Chini ya viwango vipya wenyeji wangelipa dola 10 kutembelea hifadhi za Ziwa Nakuru na Amboseli.

    Malipo ya hifadhi za Meru, Aberdare, Mt Kenya na Tsavo yangefikia dola 10 kutoka dola 3.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako