• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Benki kupewa unafuu mikopo

    (GMT+08:00) 2020-04-08 18:51:14

    Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Dk. Philip Mpango, amesema serikali itatoa unafuu wa mikopo kwa mabenki ili kukabiliana na athari za kiuchumi zitokanazo na ugonjwa wa corona.

    Aidha amesema kimeundwa kikosi kazi maalum cha wataalamu kwa ajili ya kuangalia athari za kiuchumi zitokanazo na ugonjwa huo.

    Waziri Mpango alisema kikosi hicho kinafanya kazi ya uchambuzi wa kina wa athari zinazoweza kujitokeza na kuwa kazi hiyo inatakiwa kufanyika kwa umakini.

    Alisema timu hiyo inajuyomuisha watu kutoka Zanzibar, wako katika kamati ya kitaalamu, lakini pia kwenye kamati ya kitaifa ambayo inaongozwa na Waziri Mkuu, pia katika Wizara ya Fedha imeelekeza wizara zingine za kisekta ikiwamo Benki Kuu kukutana na wadau mbalimbali kwa majadiliano mbalimbali ili wapokee mapendekezo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako