• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yahimiza ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-04-08 19:53:35

  Tangu kutokea kwa maambukizi ya virusi vya Corona, kwa kufuata mawazo ya jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na msimamo wa kuwajibika, China imetoa taarifa wazi na kwa wakati kuhusu maambukizi ya virusi hivyo, wakati huo huo imeshirikiana na jamii ya kimataifa, na kutoa misaada kwa nchi zinazohitaji. Virusi havijali mipaka na makabila, hivyo jamii ya kimataifa inapaswa kushikamana na kushirikiana ili kushinda maambukizi ya virusi, na kulinda dunia ambayo ni nyumba ya binadamu wote.

  Ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, China imetekeleza hatua kali zaidi katika pande zote. Kutokana na juhudi kubwa za pamoja za Wachina wote, hatua za kudhibiti ugonjwa huo zina mwelekeo mzuri, na hivi sasa China inaharakisha kurejesha uzalishaji na maisha ya kawaida.

  Maambukizi ya virusi vya Corona nchini China yalifuatiliwa sana na jamii ya kimataifa. Kuanzia tarehe 3 Januari, China imekuwa ikitoa taarifa kuhusu maambukizi hayo kwa Shirika la Afya Duniani WHO, mashirika ya kikanda, na nchi husika ikiwemo Marekani kila baada ya muda fulani. Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus alipofanya ziara nchini China mwishoni mwa mwezi Januari, aliipongeza China akisema, "Tangu kugunduliwa kwa virusi vya Corona, China imevunja rekodi ya kutambua virusi kwa muda mfupi zaidi. Pia China imefanikiwa kwa haraka katika utafiti wa utaratibu wa jeni ya virusi hivyo, na kuutoa utaratibu huo kwa nchi nyingine mara moja."

  Licha ya kutoa taarifa kwa wazi, China pia haikuficha chochote katika hatua za kukinga virusi hivyo, njia za kutibu wagonjwa na utafiti wa kisayansi. Hivi karibuni maambukizi ya virusi vya Corona yameenea kwa haraka katika nchi mbalimbali duniani. Nchi nyingi zinathamini uzoefu wa China katika kukinga virusi na kutiba wagonjwa. Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza wa Uturuki Profesa Yesim Tasova, alihudhuria mkutano ulioandaliwa na China kwa njia ya video kwa ajili ya kujulisha uzoefu wake wa kukabiliana na COVID-19, akisema,

  "Naona mkutano huo unanisaidia sana, na nimejifunza elimu na uzoefu mkubwa. Tuliuliza maswali, na kupata majibu mazuri. Nina hakika kwamba watu wengine waliohudhuria mkutano huo pia watanufaika."

  Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Machi, China imetoa uzoefu wa kukinga virusi na kutiba wagonjwa kwa nchi na sehemu zaidi ya 180, na mashirika zaidi ya 10 ya kimataifa na kikanda, na pia imeandaa mikutano na wataalamu wa afya wa nchi zaidi ya 100 kwa njia ya video.

  China pia imetoa misaada halisi kwa zaidi ya nchi 120 na mashirika manne ya kimataifa, na misaada hiyo ni pamoja na mask, nguo za kukinga virusi, vifaa vya kupima virusi, na mitambo ya kupumua. Licha ya hayo, China imetuma vikundi vya madaktari kwa nchi kadhaa zikiwemo Iran, Iraq, Italia, Serbia, Cambodia, Pakistan, Venezuela na Laos.

  Tarehe 21 mwezi Machi, kikundi cha madaktari 6 cha China kilifika nchini Serbia. Rais Aleksandar Vucic wa nchi hiyo aliwapokea madaktari hao kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Belgrade, na aliishukuru China na watu wa China, akisema, "Kuja kwa wataalam wa matibabu wa China kuna maana kubwa kwa Serbia kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Kwani wao ni watu pekee walioshinda virusi hivyo. Nawashukuru watu wa China. Kila Serbina inapokumbwa na majanga, wanatusaidia kama marafiki zetu wakubwa. Serbia haitasahau misaada iliyotolewa na China."

  Maambukizi ya COVID-19 yamethibitisha tena kuwa, binadamu ni jumuiya yenye hatma ya pamoja, na jamii ya kimataifa inapaswa kushikamana na kushirikiana ili ushinda ugonjwa huo. Mkuu wa Idara ya Utafiti wa Masuala kati ya Brazil na China katika Mfuko wa Vargas wa Brazil Evandro Menezes de Carvalho anasema, "Katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, kazi zilizofanywa na China ni mfano halisi wa utekelezaji wa mawazo ya jumuiya yenye hatma ya pamoja. Serikali ya China imefafanua mawazo hayo kwa hatua za kivitendo, na kutuambia kuwa sisi sote ni familia moja kubwa."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako