• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Haji Manara asema ana uwezo wa kufanya kazi FIFA

    (GMT+08:00) 2020-04-09 17:39:14

    Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa kutokana na uzoefu wa kazi alio nao, anaweza kufanya kazi katika Shirikisho la Soka Duniani FIFA kama msemaji. Manara amesisitiza kuwa hakukuwa na haja ya kufanyiwa usaili wa kazi ya Afisa Habari wa Klabu ya Simba kutokana na uzoefu wake kutokuwa na shaka. Aidha Haji Manara amezungumzia kuhusu suala la pesa za uwekezaji ndani ya klabu ya Simba, kama inavyozungumzwa na baadhi ya watu, ambapo amesema wenye haki ya kuhoji ni wanachana na mashabiki. Amesema wenye uhalali wa kuhoji kuhusu Bilioni 20 za mwekezaji wa Simba ni mashabiki wenyewe ambao walimpa timu, siyo mtu mwingine tu ambaye hana uhalali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako