• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono kithabiti WHO katika kupambana na virusi vya Corona duniani

    (GMT+08:00) 2020-04-09 19:53:35

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema China itaendelea kuunga mkono nafasi ya uongozi ya Shirika la Afya Duniani WHO katika ushirikiano wa kupambana na janga la virusi vya Corona duniani.

    Zhao amesema hayo baada ya Marekani kuishutumu WHO kuwa na mtazamo wa upendeleo. Amesema tangu mlipuko wa virusi vya Corona utokee, WHO inayoongozwa na mkurugenzi mkuu Tedros Ghebreyesus, imetekeleza wajibu wake ipasavyo, na kutumia mitazamo ya usahihi, sayansi na haki, na kufanya kazi muhimu katika kuratibu nchi mbalimbali kushirikiana kupambana na janga hilo, jambo ambalo limetambuliwa na kupongezwa sana na jamii ya kimataifa. Ameongeza kuwa virusi vya Corona sasa vinaenea kote duniani, na jamii ya kimataifa inatakiwa kuimarisha imani, kutumia nguvu kwa moyo mmoja na kusaidiana ili kushinda vita dhidi ya ugonjwa huu mkubwa wa kuambukizwa unaotishia maisha ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako