• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IOM yataka dola milioni 71.6 za kimarekani kuwasaidia wahamiaji wa Pembe ya Afrika kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-10 10:40:16

    Shirika la uhamiaji la kimataifa IOM limetoa wito wa kuchangisha dola 71.6 za kimarekani kwa mamilioni ya wahamiaji na wakimbizi wa ndani katika Pembe ya Afrika ili kuwasaidia kupambana na virusi vya Corona.

    Mkuu wa ofisi ya IOM inayoshughulikia mambo ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika Bw. Mohammed Abdiker ametoa taarifa akisema, mamilioni ya watu kwenye maeneo hayo wanakumbwa na changamoto kutokana na kufungwa kwa mipaka, zuio la kutotembea usiku, na kusimamishwa kwa shughuli za uchumi. Amesema mlipuko wa virusi vya Corona ni changamoto ya kiafya kwa wote, na inawaathiri zaidi wahamiaji kwenye kanda hiyo, ambao wanategemea kufanya kazi nje ili kumudu familia zao nyumbani.

    Ameongeza kuwa fedha hizo zitatumika katika kuimarisha usimamizi wa ugonjwa, kuboresha hatua za kinga, kuimarisha uratibu wa kuvuka mipaka, na kuwafahamisha wahamiaji na wakimbizi wa ndani jinsi ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako