• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Africa Kusini yaongeza muda wa zuio la kupambana na virusi vya Corona kwa wiki mbili zaidi

    (GMT+08:00) 2020-04-10 10:41:10

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza kuwa muda wa zuio linalotekelezwa nchini humo kwa lengo la kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona utarefushwa kwa wiki mbili zaidi.

    Akihutubia taifa kwenye televisheni, Rais Ramaphosa amesema anatambua athari za zuio hilo kiuchumi na kwa wananchi, lakini uamuzi huo haujafikiwa kwa urahisi.

    Rais Edgar Lungu wa Zambia pia ameongeza siku 14 zaidi kwa zuio la nchi hiyo, na kusema licha ya kuwa maendeleo yanapatikana katika kupambana na janga hili, tishio bado lipo. Rais Edgar Amekubali kuwa hatua hizo zimekuwa na athari mbaya kwa maisha ya wananchi na uchumi lakini ni muhimu zitekelezwe ili kuzuia ugonjwa huo.

    Ikiwa ni sehemu ya hatua za kupambana na virusi vya Corona Sudan Kusini imetoa mipango ya kutoa masomo kwa njia ya redio kwa wanafunzi katika nchi hiyo.

    Waziri wa elimu ya jumla na mafunzo wa nchi hiyo Bw. Awut Deng Achuil amesema mpango huo unaungwa mkono na wadau kama Shirika la kudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na Shirika la Elimu ya wasichana Sudani Kusini (GESS).Umoja wa Afrika waunga mkono shirika la WHO

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako