• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BASKETBALL: Corona yatibua kikapu Arusha

    (GMT+08:00) 2020-04-10 18:30:30

    Ligi ya mchezo wa Kikapo Mkoa wa Arusha iliyokuwa ianze kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu haitafanyika tena hadi itakapotangazwa baadaye. Mratibu wa Mashindano wa Chama cha Mchezo wa Kikapu Arusha Bariki Kilimba amesema, timu nane zilitarajia kuoneshana ubabe kusaka ubingwa wa mkoa, lakini mambo yamevurugika kwani baada ya kumalizika kwa Ligi ya Mkoa, ratiba ya Chama hicho ilikuwa ni kuanza maandalizi ya Kilimanjaro Cup sawa na kalenda ya Shirikisho inavyoelekeza. Bingwa wa msimu uliopita ilikuwa timu ya Kings ambayo ilikwenda kushiriki mashindano ya mabingwa wa mikoa, na TCDC iliyoshika nafasi ya pili na kushiriki mashindano ya kanda na kutwaa ubingwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako