• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bill Gates apongeza China kwa kufanikiwa kudhibiti COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-10 19:09:02

    Mwenyekiti mwenza wa Mfuko wa Gates wa Marekani Bw. Bill Gates amesema China imepata mafanikio makubwa katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona kwa kutekeleza kwa makini hatua kadhaa ikiwemo karantini, ambazo zinaiwezesha nchi hiyo ianze kufikiria kurejesha uzalishaji na masomo.

    Bw. Gates alisema hayo jana alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la China CMG kwa njia ya video. Amesema China ikiwa ni nchi ya kwanza iliyokabiliwa na virusi vya Corona, ilikumbwa na changamoto kubwa katika kipindi cha awali kutokana na kukosa ufahamu na ugonjwa huo. Lakini hivi sasa China imerejesha shughuli za uzalishaji na kutoa vifaa muhimu vya matibabu, jambo ambalo litazisaidia nchi nyingine kupambana na janga hilo.

    Bw. Gates amesema uzoefu wa China unaweza kuchukuliwa kama mfano wa kukabiliana na virusi vya Corona angalau kwa nchi zenye uwezo kama China au zile zenye uwezo mkubwa zaidi. Ametoa mfano wa mji wa New York, Marekani akisema mji huo ulishindwa kuchukua hatua mapema, na sasa hatua zinaharakishwa, lakini zitafanikiwa endapo watu wote watafuata kanuni za umbali wa kujikingia na virusi, ambazo kwa sasa hazijatekelezwa ipasavyo.

    Akizungumzia vitendo vya kutupiana lawama kati ya nchi mbalimbali kuhusiana na maambukizi ya virusi vya Corona, Bw. Gates amesisitiza kuwa ukosefu wa ushirikiano sio tu utazuia nchi hizo kukabiliana na ugonjwa wa kuambukizwa kama huu, bali pia kutaathiri utatuzi wa suala kama mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako