• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya 8 kati ya 10 wasema kufanyia kazi nyumbani hakuzai matunda

    (GMT+08:00) 2020-04-10 19:09:36
    Ripoti ya utafiti uliofanywa hivi majuzi kuhusu kitendo cha kufanyia kazi nyumbani unaonesha kuwa wakenya wanane kati ya 10 wanaamini kuwa kufanyia kazi nymbani hakuna mafanikio yoyote ya uzalishaji. Ripotri hiyo ambayo ilitoilewa na shirika la utafiti la consumer Insight inatoilewa wakati ambapo waajiri wamekuwa wakiwataka wafanyakazi wao kufanyia kazi majumbani ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona. Utafiti huo ambaop ulitolewa alhamisi unasema kuwa asilimia 81 ya wakenya walioojiwa wanaona hatua hiyo haina mafanikio yoyote katika uzalishaji. Ni asilimia ndogo tu ya walioojiwa wanaona kufanyia kazi nyumbani kunazaa matunda. Wachambuzi wa mambo ya biashara wanaona utafiti huo umeonyesha wazi kuwa uzalishaji huenda ukaathirika kwa kiwango kikubwa hasa wakati huu ambapo karibu nusu ya wafany kazi wa makampuni wanafanyia kazi majumbani mwao ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona ambapo hivi idadi ya maambukizi inadaiwa kufika 184.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako