• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Mbeya ailalamikia TPA kuhusu meli tatu

    (GMT+08:00) 2020-04-10 19:09:54
    Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini Tanzania (TPA), kituo cha Kyela mkoani humo, kuitwa kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili waeleze sababu ya meli tatu zilizojengwa ndani ya ziwa hilo kutofanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili tangu ...

    Alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambayo ilitembelea Bandari ya Kiwira, zilipoegeshwa meli hizo ambazo zimejengwa na serikali kwa zaidi ya Sh. bilioni 21 kupitia Mkandarasi mzawa Kampuni ya Songoro Marine.

    Chalamila alisema kitendo cha meli hizo zilizotengenezwa kwa gharama kubwa kuegeshwa kwenye maji kwa muda mrefu bila kufanya kazi ya uzalishaji ni hasara na kwamba ni bora TPA wangeishauri serikali isizitengeneze.

    Alisema hakuna sababu ya mizigo zikiwamo ndizi zinazozalishwa wilayani Rungwe kusafirishwa kwenda nchi jirani ya Malawi kwa kutumia magari wakati meli hizo zipo na hazifanyi kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako