• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni yatoa mafuta lita 50,000 kusaidia vita corona

    (GMT+08:00) 2020-04-10 19:10:25
    Kampuni ya Puma Tanzania imetoa mafuta lita 50,000 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana navirusi vya Corona nchini humo. Mafuta hayo yanasemekana yatatumika kwenye magari ya kubeba wagonjwa. Akipokea lita hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali inayosimamia mapambano dhidi ya ugonjwa huo amepongeza kampuni hiyo akiongeza kuwa ni ishara ya uzalendo ambao unafaa kuigwa na kila mtanzania. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Puma, Dominic Dhanah, alisema wametoa mafuta hayo yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 100 na wana imani kuwa yatasaidia kuokoa maisha ya watu. Alisema mafuta hayo yatatumika kwenye magari ya kubeba wagonjwa, hospitali na vituo mbalimbali vya afya vinavyoshughulika kuhudumia wahanga wa ugonjwa huo. Dhanah alisema Kampuni ya Puma tayari imechukua hatua mbalimbali zinazosaidia kuwakinga wafanyakazi na wateja wake dhidi ya ugonjwa huo ikiwamo kuweka maji yanayotiririka na sabuni katika vituo vyake vyote vya mafuta. Alisema kampuni ina uwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta milioni 94 na kuna vituo 56 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako