Jarida la PNAS lilichapisha makala iitwayo "Phylogenetic network analysis of SARS-CoV-2 genomes" katikati ya wiki iliyopita, inayosema aina nyingi za virusi vya Corona zinagunduliwa Marekani na Australia. Makala hiyo inaandaliwa kwa pamoja na makundi ya utafiti ya Ujerumani na Uingereza, mwandishi wa kwanza wa makala hiyo ni dokta Peter Forster kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge. Hivi karibuni CGTN ilimhoji dokta Forster kwa njia ya video, ambapo amesema hakuna ushahidi unaoonyesha virusi vya Corona vinatoka Wuhan, China.
Dokta Forster amesema lengo la utafiti huo ni kuthibitisha aina ya awali ya virus. Watafiti walichambua takwimu za jini za virusi 160 vya SARS-Cov-2 kutoka sehemu mbalimbali duniani kati ya tarehe 24, mwezi Desemba mwaka 2019 hadi tarehe 4 mwezi Machi mwaka huu, na kugundua aina tatu kuu za SARS-Cov-2 na kuzipa jina A, B, na C.
Virusi vya aina A ni vya awali, virusi vya aina B vinatoka A, na virusi vya aina C vinatoka B, na aina hizo tatu ziko katika maeneo tofauti duniani, na zina tofauti kubwa. Virusi vya aina A na C viligunduliwa zaidi katika watu wa Ulaya na wamarekani. Virusi vya aina B ni virusi vya kawaida katika Asia ya Mashariki.
Dokta Forster amesema, wakati maambukizi ya virusi vya Corona yalipogunduliwa mjini Wuhan, jini ya virusi hiyo ni ya aina B, na kwamba watafiti walikosea na kuichukulia virusi vya aina B kuwa virusi vya awali, lakini virusi vya aina A ndio virusi vya awali.
Utafiti unaonyesha kuwa, karibu nusu ya kesi za maambukizi ya virusi vya aina A ya Corona zinatoka nje ya Asia Mashariki, na wengi wako Marekani na Australia, na theluthi mbili za kesi ya Marekani ni virusi vya aina A.
Dokta Forster amesema, utafiti unaonyesha kuwa, kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya Corona huenda vinatoka kwa popo na kwenda kwa binadamu, kati ya tarehe 13, Septemba hadi tarehe 7 Desemba mwaka jana. Hivyo jini ya virusi iliyopatikana tarehe 24 Desemba mwaka jana haiwezi kueleza kwa usahihi chanzo cha ungonjwa huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |