• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mabalozi wa nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2020-04-14 18:20:17

    Jana Jumatatu, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Chen Xiaodong alikutana na mabalozi wa nchi zaidi ya 20 za Afrika nchini China kwa wakati mmoja, na kubadilishana nao maoni kuhusu hali ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona inayohusu waafrika walioko mkoani Guangdong.

    Bw. Chen amesema, Wachina siku zote wanawachukulia watu wa Afrika kuwa wenzi na ndugu wanaoweza kukabiliana kwa pamoja katika taabu na furaha. Baada ya maambukizi ya virusi vya Corona kutokea, pande mbili za China na Afrika zimeshikamana na kutatua masuala kwa pamoja. Kwa sasa maambukizi hayo yanapoenea barani Afrika, China imetoa vifaa vya kupambana na maambukizi kwa Afrika. Ili kukabiliana na changamoto kubwa za maambukizi ya virusi vya Corona, China na Afrika zinahitaji kuimarisha zaidi mshikamano kuliko wakati wowote, na zinahitaji kulinda hali ya jumla ya ushirikiano wa kirafiki kuliko wakati wowote. China itaendelea kuongeza nguvu ya kuiunga mkono Afrika kadri inavyoweza, na pia kushirikiana na Afrika kupambana na maambukizi ya virusi hivyo mpaka zipate ushindi wa mwisho.

    Bw. Chen amesema, China inazingatia sana hali ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona inayohusu waafrika walioko mkoani Guangdong. Idara husika za mkoa huo zimechukua hatua za marekebisho, kutekeleza usimamizi wa afya kwa kufuata kanuni za kutokuwa na tofauti, na kwamba kuanzia jana zimeanza kuondoa hatua za usimamizi wa afya kwa watu wa Afrika ambao hawajathibitishwa kuwa na maambukizi na walio karibu na wagonjwa hao, pia kujenga mfumo wa mawasiliano pamoja na balozi za nchi za Afrika mjini Guangzhou. Amesema serikali ya China inawatendea kwa usawa wageni nchini China, hii ni sera na msimamo wa siku zote za China.

    Ameongeza kuwa Waafrika wanatendewa kwa usawa na urafiki nchini China, na pia ametumai mabalozi wataelewa kwa usahihi hatua na sera za China, kuwafahamisha wananchi wao ukweli na kuhimiza serikali zao na wananchi wao kuelewa mambo hayo kwa usahihi. Pia amesema China inatumai serikali za nchi za Afrika zitachukua hatua za lazima kuhakikisha usalama na maslahi halali ya Wachina na mashirika na makampuni ya China katika nchi zao.

    Mabalozi wa nchi za Afrika wameishukuru China kwa kutoa taarifa za hatua zitakazochukuliwa mkoani Guangdong, na kuahidi kuwa watatoa ripoti za ukweli mara moja kwa serikali zao, na kutoa taarifa kwa raia wao walioko Guangdong. Wanatumai hatua hizo zitatekelezwa kwa ufanisi. Nchi za Afrika zinapenda kushirikiana na China kuwaongoza raia wao kufuata sheria za China na kufanya kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Mabalozi hao wanasema, Afrika na China ni ndugu na wenzi wazuri, na mambo yaliyotokea mkoani Guangdong ni masuala kati ya ndugu wa Afrika na China, na yanaweza kutatuliwa kupitia mazungumzo ya kirafiki. Nguvu yeyote ya nje, bila kujali ina lengo gani na kuchukua njia gani, haiwezi kuzuia maendeleo ya uhusiano na urafiki kati ya Afrika na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako