• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Nyota mwingine wa Marathoin wa Kenya afungiwa kwa kukiuka matumizi ya dawa za kusisimua misuli

    (GMT+08:00) 2020-04-15 12:19:06

    Bingwa wa Kenya wa mbio za Marathon ya London za mwaka 2017 Daniel Wanjiru amefungiwa kushiriki riadha kwa kutumia dawa za kusisimua misuli. Kitengo cha Uadilifu cha Wanariadha (AIU) Jumanne kilitangaza kumfungia mara moja Wanjiru kwa muda mfupi kwa kudanganya vipimo vya matumizi ya dawa za kusisimua misuli vya Wanariadha chini ya Sheria za Shirika linalopiga marufuku dawa za kusisimua misuli Duniani. Wanjiru alijibebea umaarufu wakati alipompiku mkimbiaji nguli wa mbio ndefu wa Ethiopia Kenenisa Bekele na kupata ushindi wa Marathon ya London mnamo 2017 kabla ya kumaliza wa nane katika mbio za Dunia za London mwaka 2017

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako