• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vita dhidi ya virusi vya Corona yaingia mashakani baada ya WHO kuingizwa kwenye masuala ya kisiasa

  (GMT+08:00) 2020-04-15 18:17:29

  Rais Donald Trump wa Marekani, jana ametangaza kuwa nchi hiyo itasimamisha ufadhili kwa Shirika la Afya Duniani, (WHO). Rais Trump amelilaumu Shirika hilo kwa kutotoa kwa wakati habari kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona, kutotoa mapendekezo kuhusu kinga na udhibiti wa maambukizi, na kutotangaza haraka hali ya maambukizi makubwa ya duniani. Rais Trump amenukuliwa akisema, "baada ya muda wote huu, ni wakati wa WHO kuwajibika." Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Chuo Kikuu cha John Hopkins, mpaka kufikia leo, idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona duniani imefikia 1,986,986, na watu 126,812 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

  Hadi sasa, maambukizi ya virusi vya Corona yameenea dunia nzima, usalama wa afya ya umma duniani unakabiliwa na changamoto kubwa. Lakini wakati huo huo, Marekani inaendelea kutoa lawama kwa WHO bila msingi wowote, hali ambayo inahatarisha mapambano dhidi ya virusi vya Corona kote duniani, na kuleta athari mbaya, na ni wazi kuwa itadhuru maslahi ya watu wa nchi mbalimbali, ikiwemo Marekani.

  Marekani kusitisha ufadhili kwa WHO kutaathiri vibaya uendeshaji wa Shirika hilo na hakutasaidia ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona. Mkurugenzi wa WHO Bw. Tedros Ghebreyesus hivi karibuni alisema, ni mara ya kwanza kuona maambukizi makubwa ya virusi vya Corona, na kwa nchi nyingi zinazokumbwa na hali mbaya ya maambukizi hayo, changamoto zao siyo kama wataweza kufanikiwa kukabiliana na janga hilo, bali ni wanadhamiria kiasi gani kufanya hiyo.

  Ukweli ni kwamba, serikali ya Marekani haikutilia maanani onyo lililotolewa na WHO, hivyo kuchelewa kuchukua hatua za kinga na maandalizi ya vifaa vya matibabu. Imepoteza bure muda uliopatikana kutokana na juhudi za na China na nchi nyingine, na kusababisha kushindwa kudhibiti maambukizi hayo.

  Mara kwa mara WHO inasisitiza kuwa, ushirikiano ni muhimu zaidi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, na haiwezi kupuuza nchi yeyote.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterrez hivi karibuni ametoa taarifa akisema, maambukizi ya virusi vya Corona ni moja kati ya changamoto za hatari zinazokabiliwa na dunia kwa sasa, kwani yanaleta athari mbaya kwa afya, uchumi na jamii ya binadamu, na mshikamamo na ushirikiano wa dunia ni muhimu sana. Ili kushinda vita hivyo dhidi ya virusi vya Corona, ni lazima jamii ya kimataifa iunge mkono juhudi zinazofanywa na WHO.

  Wakati huo huo, Kundi la Nchi 20 (G20) limeahidi kuunga mkono na kuimarisha kazi ya WHO katika kuratibu operesheni ya kukabiliana, na kutoa wito wa kutoa fedha zote za mpango wa WHO wa kukinga na kukabiliana na magonjwa.

  Kutokana na maambukizi hayo kuenea kwa kasi duniani, China, Uingereza na nchi nyingine zimechangia fedha kwa WHO, kuunga mkono ushirikiano wa kimataifa katika mapambano hayo, kuzisaidia nchi mbalimbali kuinua uwezo wa kukabiliana na maambukizi hayo, na kuimarisha ujenzi wa mfumo wa afya ya umma. Jumatatu, Bw. Tedros kwa mara nyingine tena alisema, katika njia mbele yetu ni lazima tushikamane, mshikamamo wa kitaifa na mshikamamo wa dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako