• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje Nigeria: Baadhi ya raia wa Nigeria walioko Guangzhou hawakufuata kanuni ya udhibiti wa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-15 18:18:09

    Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama na Balozi wa China nchini humo Zhou Pingjian jana walikutana na waandishi wa habari kwa pamoja, na kufafanua hali halisi kuhusu kile kinachoitwa "Wanigeria kutendewa vibaya mjini Guangzhou", na kutoa taarifa ya hali ilivyo sasa ya raia wa Nigeria waliowekwa karantini huko Guangzhou.

    Bw. Onyeama amesema, hivi karibuni baadhi ya raia wa Nigeria baada ya kufika mjini Guangzhou, China, walithibitishwa kuwa wameambukizwa virusi vya Corona. Mama mmoja aliyethibitishwa kuwa na virusi hivyo ni mmiliki wa mgahawa ambapo Wanigeria na Waafrika kutoka nchi nyingine wanakwenda mara kwa mara. Baada ya kubainisha hali hiyo, serikali ya China ilichukua hatua za kufunga mgahawa huo na kuwaweka karantini watu waliokuwa karibu na mgonjwa huyo. Inafahamika kuwa watu waliowekwa karantini hawaruhusiwi kurudi hotelini au kwenye makazi yao. Lakini baadhi ya Wanigeria walielewa vibaya kutokana na video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii, wakidhani Wanigeria na Waafrika walilengwa katika zoezi la kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

    Bw. Onyeama amesema, mfumo wa kuwasiliana umejengwa sasa kati ya serikali ya mji wa Guangzhou na ubalozi mdogo wa Nigeria mjini humo, ambapo pande mbili zinashirikiana kutoa ufahamu zaidi ili wahusika waelewe kuwa, hatua hizo zina lengo la kuhakikisha usalama na afya ya wakazi wote wa Guangzhou, wakiwemo raia wa nchi za nje. Waziri huyo ameongeza kuwa, hivi sasa raia wa Nigeria waliowekwa karantini mjini Guangzhou wanahudumiwa vizuri.

    Balozi wa China nchini Nigeria Zhou Pingjian amesisitiza kuwa, sera ya China ni kwa watu wote kutoka nchi za nje, na serikali ya China inapinga vitendo vinavyolenga watu wa kundi tofauti, na haivumilii kauli au vitendo vya ubaguzi wa aina yote ile. Kutokana na ushirikiano wa pande mbalimbali, masuala yanayofuatiliwa na Nigeria na nchi nyingine za Afrika yamepewa utatuzi au yanatatuliwa.

    Balozi Zhou alitaja takwimu zilizokusanywa hadi kufikia Jumatatu wiki hii, kwamba miongoni mwa kesi 26 zilizoripotiwa za wagonjwa wa virusi vya Corona waliofika mjini Guangzhou kutoka nchi za nje, 19 ni Waafrika, wakiwemo Wanigeria 9. Pia miongoni mwa wageni 60 waliothibitishwa kuambukizwa ambao hawajaonyesha dalili yoyote, 57 ni Waafrika. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, raia wa nchi za Afrika wakiwemo Wanigeria walioko Guangzhou wanakabiliwa na hatari ya kiwango cha juu kuambukizwa virusi vya Corona, hivyo maana inapaswa kuchukua hatua ya kuwapima afya, ambayo inalenga kuwalinda kiafya wakazi wote wa mji huo wakiwemo Waafrika. Balozi Zhou amesisitiza kuwa, hatua hizo zimechukuliwa kwa watu wote wanaokabiliwa na hatari ya kiwango cha juu ya kuambukizwa virusi vya Corona, na watu elfu 15 wameshawekwa karantini katika makazi yao au hoteli maalumu, na miongoni mwao wageni kutoka nchi mbalimbali duniani ni zaidi ya 4,600.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako