• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei ya mafuta yashuka Kenya

    (GMT+08:00) 2020-04-15 19:00:13

    Mamlaka ya kuthibiti bei ya kawi nchini Kenya imepunguza bei ya kawi ili kupunguza shinikizo kwa wakenya wakati huu serikali ikipambana na virusi vya Corona.

    Bei ya petrol inapunguzwa kwa shilingi 18, mafuta ya taa shilingi 18.8 na dizeli shilingi 4.

    Punguzo hilo linatarajiwa kusaidia sekta ya uchukuzi wa bidhaa na abiria kufuatia agizo la serikali la kupunguza abiria wanaosafiria kwenye mabasi.

    Mwezi uliopita waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe aliagiza mabasi yanayobeba abiria 14 kubeba watu 8 tu ili kutimiza hitaji la mwanya wa mita moja kati ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako