• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: Nzige wahatarisha usalama wa chakula Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-04-15 19:00:54

    Umoja wa mataifa unaripoti kuwa nzige wameharibu zaidi ya ekari 500,000 za chakula ncnini Ethiopia na huenda watu milioni 1 wakakabiliwa na njaa katika nchi hiyo ya upembe wa Afrika.

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO lisema utafiti wake nchini Ethiopia umebaini kuwa makundi mapya ya nzige hao wa jangwani watasababisha hasara kubwa.

    Nchini Ethiopia, wadudud hao wamesababisha uharibifu mkubwa wa mtama, mpunga na mahindi.

    Tayari nzige hao wamesababisha uharibifu wa chakula la lishe la mifugo nchini Ethiopia, Somalia, Kenya, Djibouti, Eritrea, Tanzania, Sudan, Sudan Kusini na Uganda.

    Zaidi ya watu milioni 8.5 nchini Ethiopia wanakabiliwa na njaa mbali na kuwepo kwa nzige, kulingana na FAO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako