• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Dickson Etuhu afungiwa miaka mitano kwa kupanga matokeo

    (GMT+08:00) 2020-04-17 08:26:36

    Mchezaji wa zamani wa Man City Dickson Etuhu, 37, amefungiwa miaka mitano kujihusisha na soka kutokana na kubainika kuwa alihusika kupanga matokeo ya mechi Mei 2017. Etuhu alihusika kupanga matokeo baada ya kubainika kuwa alimshawishi mchezaji mwenzake wa AIK Stockholm anayejulikana kwa jina la Kane Stomatopoulos kupanga matokeo katika mchezo dhidi ya Gothenburg. Inaaminika kuwa golikipa Stomatopoulos alipewa ofa ya pauni 180,000 na Etuhu ili acheze chini ya kiwango mchezo huo baada ya golikipa namba moja wa timu hiyo kuumia na kuukosa mchezo huo. Etuhu alikana mashitaka hayo ila baada ya uchunguzi wa kina Novemba 2019 alibainika kufanya kosa hilo hivyo sasa chama cha soka Sweden kinamfungia miaka mitano kucheza soka ambapo adhabu hiyo itamfanya asiwe na nafasi ya kucheza soka nchi za Scandinavian hadi Aprili 13 2025.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako