• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Lineker, Neville waipongeza Manchester United

    (GMT+08:00) 2020-04-17 16:03:00

    Uongozi wa klabu ya Manchester United umepongezwa kwa kuchukua hatua ya kuzipunguza mwanga baadhi ya herufi za maandishi kwenye neno Manchester lililoandikwa uwanja wa Old Trafford na kubakia herufi HNS UNITED. Uongozi wa Manchester United umechukua hatua hiyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wafanyakazi wanaopambana na virusi vya Corona. Pongezi hizo zimetolewa na magwili wa soka la England Gary Lineker na Gary Neville kwa kusema inapendeza na kutia moyo kwa mashabiki wa klabu hiyo, ambao pia wameungana na watu wote duniani kupambana na Virusi vya Corona. Wawili hao wamesema Manchester United ni klabu kubwa na maamuzi yaliyochukuliwa na uongozi wake, yanadhihirisha ni vipi walivyoguswa na tatizo linaloendelea kuiandama dunia kwa sasa. Maeneo mengine nje ya uwanja wa Old Trafford, yamewashwa taa za bluu ili ziendane na rangi ya mfumo wa huduma ya afya nchini England.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako