• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Safaricom yachangia hazina ya dharura ya kukabilian na Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-17 18:45:48
    Kampuni ya mawasiliano ya simu nchini Kenya Safaricom imeahidi kutoa jumla ya shilingi milioni 200 kusaidia wakenya masikini kupata chakula ikiwa ni mchango wake kwa hazina ya dharura ya kukabiliana na janga la Corona. Kampuni hiyo imesema hivi sasa jumla ya mchango wake katika vita dhidi ya Corona ni bilioni 5.7.Makampuni mengi pia yametoa michango yao ukiwemo mchango wa jumla ya shilingi milioni 70 kutoka kwa muungamo wa wafanya biashara mjini Nairobi.Kampuni zingine ambazo zimechangia hazina hiyo ni pamoja na Reckitt and Benckiser, PZ Cussons, Live Ad, Unilever, Menengai, Copia, Rotary International, Johnson and Johnson, Swiss Development Cooperation (SDC), Twiga, Chandaria, na Microsoft. Shirika linguine ambalo pia limetoa mchango wake ni wakfu wa Jac Ma ambao ulitoa msaada wa vifaa vya kupimia wagonjwa pamoja na mask ambazo zitasaidia kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona nchini Kenya. Wafanya biashara wengi wameendelea kupata hasara huku wengi wakihimiza jamii kuchukua tahadhari na kushirikiana katika kutokomeza ugonjwa huo wa Covd 19.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako