• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasaidia nchi za Sahel kupambana na Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-17 18:46:08
    Shirika la fedha la kimataifa IMF limeidhinisha msaada wa dharura wa jumla ya dola milioni 230 kuzisaidia nchi za ukanda wa Sahel kupambana na virusi vya Corona.Bodi ya shirika hilo limesema jumla ya dola milioni 115.3 zitakabidhiwa nchi ya Burkina Faso na nyingine 114.5 zikipelekwa nchini Niger kupambana na janga la Corona ambalo linaendelea kuwaangaisha waafrika wengi hivi sasa.IMF pia imesema itaondoa madeni yote kwa nchi hizo. Nchi hizo ambazo ni miongoni mwa nchi maskini duniani zimekuwa zikikabiliwa na changmoto ya vita vinavyotekelezwa na wapiganaji wa kiislamu ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha wengi bila makao. IMF pia imetangaza msaada wa dharura kwa nchi ya Ghana na nyingine dola milioni 442 kwa nchi ya Senegal kusaidia juhudi zake za kupambana na virusi vya Corona.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako