• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pato la taifa la China lapungua kwa asilimia 6.8 katika robo ya kwanza ya mwaka kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-04-17 20:16:04

  Pato la ndani la China (GDP) limefikia dola za kimarekani trilioni 2.91 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni chini kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

  Mamlaka ya Takwimu ya China (NBS) imesema, maendeleo ya uchumi na jamii nchini China yameshuhudia utulivu katika kipindi hicho, huku ikikiri kuwa mlipuko wa virusi vya Corona umeleta tishio kubwa. Mamlaka hiyo imesema, hali ya kudhibiti na kuzuia mlipuko imeendelea kuboreka, na kwamba kuanza tena kwa kazi na uzalishaji kumeongezeka kwa kasi na viwanda vya kimsingi vinaendelea kukua kimsingi.

  Wachambuzi wanasema, matokeo haya si ya kushangaza katika kipindi hicho cha mwaka 2020, ambapo China ilikabiliwa na changamoto kubwa zinazotokana na maambukizi ya virusi vya Corona, na kutoa kipaumbele katika kufanya kila iwezalo kuokoa maisha ya raia wake. Kwa hiyo, China ilichukua hatua kali za kudhibiti kuenea kwa virusi, kupunguza safari za watu na shughuli za kiuchumi na kijamii, na kufanikiwa kudhibiti virusi ndani ya muda mfupi, na ni jambo lisiloepukika kwamba, hatua hizo zinasababisha kushuka kwa kasi ya uchumi.

  Wakati huohuo, virusi vinaenea katika nchi mbalimbali duniani, na kusababisha kupungua sana kwa uwekezaji wa kimataifa, biashara ya uchukuzi na mawasiliano ya watu, na nchi na mashirika mengi yamepunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi. Katika mazingira haya magumu, uchumi wa China hauwezi kuwa wa tofauti.

  Hata hivyo katika miezi miwili iliyopita, China ilijitahidi kuokoa maisha na uchumi kwa wakati mmoja, na kupata ufanisi wa kiasi. Hivi sasa hali ya maambukizi ya virusi vya Corona inadhibitiwa nchini China, na uchumi umeanza kufufuka kwa kasi inayozidi kuwa kubwa, jambo ambalo limeonekana kwenye viashiria vikuu vya uchumi kwa mwezi Machi.

  Wachambuzi wametoa tahadhari kuwa, China inatakiwa kujiandaa vizuri kukabiliana na hatari za nje kwa muda mrefu zinazotokana na kushuka kwa uchumi wa dunia na kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu na sintofahamu. Lakini China ina imani kutafuta fursa zinazotokana na janga hilo na kuongeza kasi ya kufufua uchumi wake ili kuendelea kuchangia utulivu wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako