• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za Afrika zafurahia misaada ya China katika kukabiliana na COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-04-19 17:33:23

  Hivi karibuni, licha ya vikundi vya madaktari vilivyotumwa na China katika nchi za Afrika, misaada ya vifaa vya matibabu dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 iliyotolewa na China pia imefurahiwa na nchi za Afrika.

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana alipoadhimisha miaka 40 tangu kupata uhuru kwa nchi hiyo aliishukuru China kwa kuipatia misaada muhimu nchi hiyo kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, na kusema juhudi za kukabiliana na virusi hivyo haziwezi kukosa misaada ya jamii ya kimataifa.

  tarehe 17, shehena ya pili ya msaada wa vifaa vya matibabu uliotolewa na kampuni ya China ilifikishwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Juba, nchini Sudan Kusini. Kwa niaba ya serikali ya Sudan Kusini, balozi wa nchi hiyo nchini China John Andruga Duku ameishukuru China kwa kutoa msaada tena, na kusema misaada hiyo inaonesha kuwa China inatilia maanani sana uhusiano kati ya nchi hizo mbili na ushirikiano kati ya China na Afrika.

  Siku hiyo shehena ya pili ya msaada wa vifaa vya matibabu uliotolewa na kampuni ya China pia ilifikishwa nchini Lesotho. Waziri wa afya wa nchi hiyo Nkaku Kabi amesema, msaada huo una maana kubwa kwa juhudi za kupambana na COVID-19 nchini humo, anaamini kuwa kwa kushirikiana na China, Lesotho itashinda ugonjwa huo.

  Siku hiyo hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya matibabu uliotolewa na serikali ya China kwa Sao Tome and Principe ilifanyika mjini Sao Tome. Waziri wa afya wa nchi hiyo Edgar Neves amesema, urafiki wa dhati hutambuliwa wakati wa taabu, msaada wa China ni muhimu sana kwa nchi hiyo katika kukabiliana na virusi vya Corona.

  Guinea-Bissau jana ilipokea msaada wa vifaa vya matibabu uliotolewa na serikali ya China. Katibu wa mamlaka ya usimamizi wa hospitali wa nchi hiyo Cornelia Aleluia Lopes Man amesema China ni mshirika muhimu asiyekosekana wa maendeleo, kwa sababu inapatikana kila wakati na kuwa pamoja na Guinea-Bissau.

  Virusi havijali mipaka, na ni adui wa pamoja wa binadamu. China na nchi za Afrika zinatakiwa kushirikiana vizuri ili kushinda virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako