• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa mawaziri wa afya wa G20 wafanyika kwa njia ya video

  (GMT+08:00) 2020-04-20 09:27:48

  Mkutano wa mawaziri wa afya wa kundi la nchi 20 (G20) umefanyika jana usiku kwa njia ya video. Mkurugenzi wa Kamisheni ya afya ya taifa ya China Bw. Ma Xiaowei ametoa wito kuwa kundi la G20 kuendelea kuliunga mkono Shirika la Afya duniani WHO kufanya kazi ya uongozi na uratibu katika kukabiliana na dharura za afya ya umma duniani.

  Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Kamisheni ya afya ya taifa ya China Bw. Ma Xiaowei amesema baada ya juhudi za miezi mitatu, hivi sasa mlipuko wa virusi vya Corona nchini China umedhibitiwa, uzalishaji mali na maisha ya wananchi vinarejeshwa kwenye utaratibu wa kawaida, lakini China haijalegeza hatua zake za kuzuia kuenea kwa virusi. Tangu maambukizi yalipoibuka, China siku zote inashikilia msimamo wa wazi na wa kuwajibika, kutoa taarifa kwa wakati kwa jumuiya ya kimataifa ikiwemo WHO. Pia amelitaka kundi la G20 kuendelea kuunga mkono taratibu za pande nyingi, kuendelea kuunga mkono WHO kufanya kazi ya uongozi na uratibu katika kukabiliana na dharura za afya ya umma duniani.

  (sauti 2)

  "Tunatoa mwito kwa nchi za G20 kushirikiana katika kuinua uwezo wa kuzuia, kudhibiti na kutibu ugonjwa wa COVID-19 kwa kulingana na hali halisi ya nchi zao. Pia zinapaswa kufanya ushirikiano katika utafiti wa dawa na chanjo ya virusi hiyo, ili kuzuia kwa ufanisi kuenea kwa virusi hivyo kati ya nchi. Tunaitaka jumuiya ya kimataifa ishikamane kupinga kithabiti uvumi, unyanyapaa na ubaguzi."

  Bw. Ma amependekeza kundi la nchi 20 kushirikiana kuzisaidia nchi zenye mifumo dhaifu ya afya, kuinua uwezo wa kukabiliana na maambukizi. China itaendelea kutoa taarifa mpya kuhusu COVID-19 kupitia mtandao wa Internet, kuendelea kutoa mipango ya kinga na tiba, na kuendelea kutoa msaada kwa nchi zenye mahitaji kadiri iwezavyo.

  Katibu mkuu wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema anafurahi kuona kuwa nchi za G20 zinapanga kulegeza hatua za udhibiti wa kijamii. Amesisitiza kuwa kuondoa hatua za zuio hakumaanishi kutokomezwa kwa maambukizi katika nchi hizo, bali ni mwanzo wa kipindi kijacho.

  (sauti 3)

  "katika kipindi kijacho, ni muhimu kwa nchi mbalimbali kuelimisha na kuhamasisha wananchi wao kupambana na maambukizi. Ili kuepuka mlipuko wa virusi kutokea tena, ni lazima kuhakikisha nchi hizo zina uwezo wa kugundua na kuthibitisha maambukizi. Cha muhimu zaidi katika kipindi kijacho ni kwamba nchi hizo zinaweza kufuatilia kila mgonjwa, kupima kila mtu anayeshukiwa kuambukizwa na kuhakikisha mfumo wa matibabu una uwezo wa kuwapokea wagonjwa kwa wakati. "

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako